Gossip

Willy Paul Aanikwa Mitandaoni kwa DM za Muda Mrefu Bila Maelezo

Willy Paul Aanikwa Mitandaoni kwa DM za Muda Mrefu Bila Maelezo

Staa wa muziki Willy Paul ameanikwa mitandaoni na dancer wa kike anayejulikana kama Nasieku, baada ya kufichua kuwa amekuwa akimtumia jumbe binafsi kwenye mitandao ya kijamii kwa takribani miaka mitatu mfululizo.

Nasieku amesema kuwa licha ya ujumbe huo kujitokeza mara kwa mara kwenye DM zake, hajawahi kuelewa dhamira halisi ya msanii huyo. Mrembo huyo ameongeza kuwa Willy Paul ndiye msanii pekee maarufu aliyewahi kumtumia ujumbe wa namna hiyo, jambo alilolitaja kuwa la kipekee na lenye kushangaza.

Wakati huo huo, mashabiki mitandaoni wamegawanyika kuhusu kauli ya Nasieku, ambapo baadhi wanahoji huenda ni kiki ya kutangaza wimbo mpya wa Willy Paul pamoja na Okello Max huku wengine wakidai kuwa labda msanii huyo wa ngoma ya My Lady amekuwa akimzimia kimapenzi dancer huyo wa kike kisiri.

Hata hivyo, hii siyo mara ya kwanza kwa Willy Paul kuanikwa mitandaoni kwa mada zinazohusiana na mahusiano ya kimapenzi. Hapo awali, amewahi kugonga vichwa vya habari mara kadhaa kwa tuhuma na madai kama hayo kutoka kwa wanawake tofauti.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *