
Staa wa muziki nchini Willy Paul ametoa changamoto kwa kampuni ya Safaricom kuongeza mirabaha yake ya Skiza tune.
Kupitia insta story yake kwenye mtandao wa Instagram Willy Paul ameshangazwa na hatua ya kampuni ya Safaricom kushindwa kuongeza mirabaha yake kupitia mpango wa skiza tune licha ya rais uhuru kenyatta kutoa agizo kwa makampuni yanayotumia kazi za wasanii kuwaongeza mirabaha yao.
Hitmaker huyo wa ngoma ya “Chocolate” amewatolea uvivu wasanii wa kenya kwa kusalia kimya kuhusu ishu ya skiza tune huku akisema kwamba wameshindwa kupigania haki zao na badala yake wanaendelea kujihusisha na masuala yasiyokuwa ya msingi.
Utakumbuka mapema mwezi huu Rais Uhuru Kenyatta kutia saini mswada wa marekebisho kuhusu hakimiliki kuwa sheria ambao utawawezesha wasanii kupata hadi asilimia 52 ya mapato yanatokana na kazi zao.
Katika sheria hiyo mpya watoa huduma wa viwango vya malipo watapata asimilia 5 ya mapato yatakayokusanywa kutokana na kazi za wasanii huku mtoa huduma za mawasiliano akiambulia asilimia 39.5.
Msanii husika sasa anatarajiwa kupata asilimia 55 ya mapato huku akiruhusiwa pia kufanya mazungumzo na watoa huduma na kuongeza kiwango hicho kutoka asilimia 52 kulingana na makubaliano baina yao na watoa huduma husika.