Gossip

Willy Paul Akataa Pambano la Ndondi na Shakib, Amwaga Hasira Kwa Diamond

Willy Paul Akataa Pambano la Ndondi na Shakib, Amwaga Hasira Kwa Diamond

Msanii wa Kenya, Willy Paul, amekataa ombi la kushiriki pambano la ndondi na Shakib Khan, mume wa mfanyibiashara na socialite maarufu wa Uganda, Zari Hassan.

Kwa mujibu wa Willy Paul, hana sababu ya kupigana na Shakib kwani ugomvi wake halisi upo na Diamond Platnumz, aliyewahi kuwa mpenzi wa Zari na baba wa watoto wake. Mkali huyo wa ngoma ya Ahere, ameeleza kwamba hana mpango wa kugeuza masuala ya kifamilia kuwa kiki za ndondi, bali anaona changamoto hiyo haina msingi kwake.

Kauli ya msanii huyo inakuja mara baaada ya Shakib kuwapa wasanii wa Kenya changamoto ya kuingia naye ulingoni kama njia ya kuonesha kuwa bado ana nguvu licha ya kichapo alichopokea Uganda hadi akapoteza fahamu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *