
App namba moja kwa huduma ya muziki Barani Afrika, Boomplay imemtaja msanii Willy Paul kuwa ndio mwanamuziki aliyesikilizwa zaidi nchini.
Kwa mujibu wa taarifa na takwimu rasmi za muziki mwaka 2021 kutoka Boomplay Willy Paul ambaye ana zaidi ya streams millioni 17.1 amekamata namba moja akiwapiku wasanii kama Rayvanny, Bahati, Otile brown,Diamond platinumz na Mbosso.
Hata hivyo Willy Paul ameshindwa kuficha furaha yake kwani ametumia ukurasa wake wa Instagram kuwashukuru mashabiki kwa kuzisupport kazi zake za muziki huku akiwahimiza waendelee kustream album yake mpya African Experience kupitia App ya Boomplay.
Taarifa hiyo iliyowekwa kwenye ripoti maalumu kuhusu muziki imeegemea zaidi kwenye data kutoka kwa app hiyo ya muziki ambayo kwa mwezi ina wastani wa watumiaji milioni 50 ulimwenguni kote.