
Nyota wa muziki barani Afrika Wizkid ametajwa kama msanii bora wa Afrika kwenye tuzo za Apple Music ambazo orodha ya washindi imetajwa nomvemba 30 mwaka huu.
Kwenye tuzo za mwaka huu Apple Music walileta kipengele kipya cha ‘Regional Artist of the Year’ ambapo kwa upande wa Afrika ametajwa mkali huyo toka nchini Nigeria.
Mshindi wa Kipengele hicho anatunukiwa kutokana na mchango wake chanya kwenye kukuza utamaduni lakini pia kufanya vizuri katika chati zao kwenye mipaka anayotokea.
Hafla za ugawaji wa Tuzo hizo za msimu wa tatu zitafanyika Disemba 7 mwaka huu.