Entertainment

YKEE BENDA ADAI HATAWAHI FILISIKA KIUCHUMI

YKEE BENDA ADAI HATAWAHI FILISIKA KIUCHUMI

Msanii Ykee Benda ni moja kati ya wanamuziki wanaofanya vizuri kwenye tasnia ya muziki nchini Uganda.

Ykee Benda anamiliki lebo ya muziki iitwayo Mpaka Records lakini pia ana kampuni ya Mpaka marketing ambaye juzi kati ilimsaidia msanii Lydia Jazmine  kulamba dili nolo la ubalozi wa bidhaa za urembo ya ngozi ya Movit.

Sasa akiwa kwenye moja ya Interview Ykee Benda amejinasibu kwa kusema kwamba hatawahi fulia kiuchumi kwa sababu ana vyanzo mbadala vya kuingiza kipato kando na muziki.

Bosi huyo wa Mpaka Records amewashauri wanamuziki wengine kuwekeza kwenye biashara ndogo ndogo kwa ajili ya kujipatia kipato ambacho kitawasaidia kusukuma mbele gurudumu la maisha.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *