Entertainment

YOUNG LUNYA ATHIBITISHA KUFANYA NGOMA MBILI NA DIAMOND PLATINUMZ

YOUNG LUNYA ATHIBITISHA KUFANYA NGOMA MBILI NA DIAMOND PLATINUMZ

Msanii wa Hip Hop kutoka nchini Tanzania, Yong Lunya amesema yeye na Diamond Platnumz wamepanga kurekodi nyimbo mbili pamoja ambazo kila mmoja atakuwa na yake.

Kauli ya Lunya inakuja mara baada ya wawili hao kukutana Afrika Kusini ambapo wote walienda kwa ajili ya maandalizi ya albamu zao na ikasemekana huwenda walirekodi ngoma.

Akizungumza katika Podcast ya Swahili Radio, Lunya amesema muda wowote watarekodi.

Young Lunya atakuwa Rapa mwingine wa kizazi kipya kufanya kazi na Diamond mara baada ya Young Killer ambaye alishirikishwa kwenye wimbo uitwao Pamela ambao unapatikana kwenye albamu yake, A Boy From Tandale iliyotoka Machi mwaka wa 2018.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *