
Mwanamuziki kutoka uganda , Ziza Bafana ametia nia ya kujitosa kwenye siasa mwaka wa 2026.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram Bafana amethibitisha kuwania ubunge kwenye uchaguzi mkuu ujao nchini Uganda kwani ana vigezo vyote vya kuwaongozi wakaazi wa masaka.
Ziza Bafana ambaye alipigia upatu Bobi wWine kutua urais nchini Uganda amesema atawania wadhfa wa ubunge kupitia tiketi ya chama cha NUP.
Mwaka wa 2021 wanamuziki wengi walipata nyadhfa mbali mbali za kisiasa baada ya wananchi kuwapigia kura kwa wingi.