Msanii mkongwe wa muziki wa Taarab, Khadija Kopa, ameweka wazi msimamo wake kuhusu madai ya kuwepo kwa ususiaji wa muziki wa Bongo Fleva, akisisitiza kuwa hakuna mtu aliyesusia muziki huo bali ni wasanii wenyewe wanaojijengea hofu bila sababu ya msingi.
Akizungumzia hali ya sasa ya tasnia ya muziki nchini Tanzania, Khadija amesema wasanii hawapaswi kuogopa, bali waendelee kufanya kazi zao kwa bidii na kuamini wanachokifanya.
Ameongeza kuwa muziki mzuri hujipatia mashabiki wenyewe bila kulazimishwa, akisisitiza kuwa kila mtu ana uhuru wa kufanya anachotaka, ikiwemo kusikiliza au kutosikiliza muziki fulani.