Instagram imefanya maboresho mapya kwenye jukwaa lake kwa kuongeza ukubwa wa picha zinazoweza kupakiwa kwenye post za kawaida.
Kwa sasa, watumiaji wanaweza kuchapisha picha kubwa zaidi ya kipimo cha kawaida cha mraba (1:1), kwa kutumia uwiano wa hadi 4:5, yaani picha ndefu kwa upande wa wima. Mabadiliko haya yanakusudia kutoa nafasi zaidi ya ubunifu, hasa kwa maudhui ya kibiashara, sanaa, mitindo na uandishi wa hadithi kupitia picha.
Katika taarifa yao rasmi, Instagram imesema kuwa lengo ni kuruhusu watumiaji kujieleza kwa njia bora zaidi na kuwapa watazamaji wao uzoefu wa kuona ulioimarishwa.
Mabadiliko Muhimu:
- Ukubwa mpya wa picha: hadi 1080 x 1350 pikseli
- Unatumika kwenye post za kawaida kwenye ukurasa wa mbele (feed), si tu Stories au Reels
- Unaboresha muonekano wa picha kwenye simu za mkononi
Hili ni jambo la kufurahisha kwa wabunifu wa maudhui, wapiga picha, na wafanyabiashara wadogo wanaotegemea Instagram kama chombo cha mawasiliano na masoko.