Content creator kutoka Kenya, Keranta, ameibuka na kuwatolea uvivu wakosoaji wake baada ya video yake ikimuonesha akitafuna jaba kusambaa mitandaoni.
Video hiyo ilisababisha gumzo kubwa, ambapo baadhi ya watu walimkosoa wakidai haifai kwa mwanamke kujihusisha na jaba ikizingatiwa kuwa asilimia kubwa ya watu wanaotumia ni wanaume.
Kupitia instastory, mrembo huyo amepuuza ukosoaji huo na kueleza kuwa kila mtu ana uhuru wa kujiburudisha anavyotaka.
Lakini pia amekanusha dhana kwamba matajiri hawatumii jaba, akibainisha kuwa hata watu wenye uwezo kifedha katika maeneo ya Pwani wanajihusisha nalo.
Jaba, ni majani ya mmea Catha edulis yanayotafunwa kwa burudani. Yana kemikali ya cathinone inayomfanya mtumiaji kuwa macho na mchangamfu, ingawa matumizi yake ya muda mrefu yanaweza kusababisha madhara kiafya na utegemezi.