Msanii Stevo Simple Boy amewashukuru mashabiki wake na wote waliomuunga mkono baada ya kutangazwa mshindi wa tuzo ya ‘Most Fashionable Inspirational Personality’ nchini Kenya.
Kupitia ukurasa wake wa mitandao ya kijamii, Stevo amesema kuwa hakutarajia kabisa kuibuka mshindi katika kipengele hicho, akieleza kuwa awali aliona kama ushindani ulikuwa mkubwa na hakujiona kama angechaguliwa. Hata hivyo, ameshukuru kwa upendo na kura nyingi alizopokea kutoka kwa watu wanaomwamini na kuthamini safari yake.
Stevo amesema ushindi huo unampa nguvu mpya ya kuendelea kujituma katika kazi yake ya muziki na kuwatia moyo wale wanaomfuatilia kwamba ndoto zinatimia pale mtu anapovumilia, kuamini na kufanya kazi kwa bidii.
Mashabiki wake wamejitokeza kwa wingi kumpongeza, wakisema kuwa Stevo anastahili tuzo hiyo kutokana na unyenyekevu wake na mtindo wake wa kipekee unaovutia watu wa rika mbalimbali.