Google Chrome inajaribu kipengele kipya ambacho kitawapa watumiaji udhibiti zaidi juu ya taarifa zao za mahali walipo mtandaoni. Kipengele hiki kinakusudia kuzuia websites kuweza kuona eneo kamili la mtumiaji.
Kwa kawaida, Chrome inaweza kupata eneo lako kupitia IP Address yako na sensa za GPS zilizopo kwenye kifaa chako. Hii inamaanisha kwamba, bila kuzingatia mipangilio ya faragha, websites unazozitembelea zinaweza kugundua mahali ulipo kwa usahihi.
Mfumo mpya utatumia njia ya “approximate location”, ambapo badala ya kuonyesha mahali halisi ulipo, Chrome itaonyesha eneo la karibu tu. Lengo la mfumo huu ni kuboresha usalama wa taarifa za mtumiaji na kuepusha websites kufahamu mahali halisi ulipo, hatua ambayo ni muhimu kwa watumiaji wanaojali faragha yao.
Kipengele hiki tayari kipo kwenye browser ya Safari, ambacho huficha hata IP Address ya mtumiaji, na hivyo kuongeza usalama zaidi. Chrome kuanza kutumia mfumo huu ni hatua muhimu kuelekea faragha yenye nguvu kwa watumiaji wake.