Msanii wa Bongo Fleva Harmonize ameonekana kuzima kabisa minong’ono mtandaoni iliyodai kuwa ameachana na mpenzi wake Kajala Masanja, baada ya kuposti video inayowaonyesha wawili hao wakiwa pamoja gym.
Katika video hiyo kupitia Instastory, Harmonize ameonekana akifanya mazoezi ya push up huku akiwa amembeba Kajala mgongo mwake, tukio lililowafanya mashabiki wengi kuona wazi kuwa bado wapo pamoja na mahusiano yao yako imara, kinyume na tetesi zilizokuwa zikisambaa.
Kwa video hiyo ya gym, Harmonize ameonekana kutuma ujumbe usiohitaji maelezo mengi, akionyesha kuwa bado yupo karibu na Kajala na kwamba uvumi unaosambazwa mitandaoni hauna msingi.
Hatua hiyo imekuja siku moja tu baada ya Kajala kuposti picha ya Harmonize akiwa kwenye tukio lao la kuvishana pete ya uchumba ndani ya yacht, jambo lililowashangaza wengi. Picha hiyo iliwaziba midomo wamebea hasa ikizingatiwa kuwa tangu tukio la kuvishana pete, wawili hao hawaja postiana tena mtandaoni, hali iliyochochea madai kuwa huenda penzi lao lilikuwa limeingiwa na ukungu.