Msanii wa Bongo Fleva, Gachi, amelazika kuomba radhi hadharani baada ya kuibua sakata la msanii Yammi kumuibia mwanaume wake ambaye alikuwa muhimili mkuu katika maisha.
Akizungumza na waandishi wa habari, Gachi amekiri kukosea na kueleza kuwa alichokifanya kilikuwa ni uamuzi wa haraka uliotokana na hasira na maumivu ya kihisia. Amewaomba radhi Yammi, mashabiki wake pamoja na Watanzania kwa ujumla kwa kuzua taharuki mtandaoni iliyomchafua Yammi mbele ya umma.
Sakata hilo lilianza pale Gachi alipotumia mitandao ya kijamii kumshutumu Yammi kwa madai ya kuingilia mahusiano yake. Kadri presha ilivyoongezeka, mgogoro huo ulihamia kwenye mkondo wa kisheria.
Inadaiwa kuwa Yammi alichukua hatua za kisheria kupinga madai hayo kwa kile kilichoelezwa kuwa ni kuchafuliwa kwa jina na taswira yake ya kisanii. Gachi naye alichukua wakili kujibu hoja hizo, hali iliyofanya wawili hao kujiandaa kwa mapambano ya mahakamani.