Mwanamuziki kutoka Uganda, Pallaso, amemtolea maneno mazito hasimu wake, Bebe Cool, akidai bosi huyo wa Gagamel hana tena nafasi katika tasnia kutokana na kiwango cha muziki wake kushuka.
Pallaso, ambaye ni mdogo wake na nguli Jose Chameleone, amesema kuwa kwa kipindi cha takriban miaka mitano iliyopita, Bebe Cool hajapata mafanikio yoyote ya maana katika muziki na amebaki kuonekana kama mtu wa kawaida.
Msanii huyo ameenda mbali zaidi na kudai kuwa Bebe Cool hawezi kamwe kulinganishwa na kaka yake, Jose Chameleone kwenye mafanikio ya muziki, kwani ni msanii wa kawaida tu ambaye amepoteza ushawishi kwenye tasnia.
Kulingana na Pallaso, Bebe Cool amepoteza ushawishi wake kimuziki (relevance) na anatumia tu majukwaa ya kisiasa ili kubaki midomoni mwa watu, huku akishindwa kutoa ngoma zinazoweza kushindana na kazi za bosi wa Leone Island (Chameleone).