Entertainment

Dr. Dre Aingia Kwenye Orodha ya Mabilionea Duniani

Dr. Dre Aingia Kwenye Orodha ya Mabilionea Duniani

Mkali wa muziki wa hip-hop na mfanyabiashara maarufu Dr. Dre amefikia rasmi hadhi ya bilionea kulingana na orodha ya mabilionea ya mwaka 2026 iliyotolewa na Forbes.

Kwa mujibu wa jarida hilo, Dr. Dre ambaye anashika nafasi ya 3,332 duniani, sasa anaungana na kundi dogo la watu mashuhuri katika sekta ya burudani ambao wamevuka thamani ya dola bilioni moja. Forbes inasema ni wasanii 22 pekee wa burudani waliowahi kufikia kiwango hicho hadi sasa.

Katika sekta ya muziki, Dr. Dre anakuwa mwanamuziki wa sita kuingia katika orodha hiyo ya mabilionea, akijiunga na majina makubwa kama Jay-Z, Beyoncé, Taylor Swift, Bruce Springsteen na Rihanna.

Utajiri mkubwa wa Dr. Dre unatokana kwa kiasi kikubwa na mafanikio ya kampuni ya vifaa vya sauti ya Beats by Dre, ambayo aliianzisha pamoja na Jimmy Iovine. Mwaka 2014, wawili hao waliiuza kampuni hiyo kwa kampuni ya teknolojia Apple kwa takribani dola bilioni 3. Baadaye chapa hiyo iliunganishwa na huduma ya muziki ya Apple Music.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *