
Mkongwe wa muziki wa Hiphop ambaye pia ni muigizaji na muandaaji wa filamu kutoka Marekani, 50 Cent, ameeleza mwaka huu anaachia ngoma mpya, series mpya pamoja na filamu mpya.
50 Cent ambaye jina lake halisi ni Curtis James Jackson ameandaa series na filamu kama, Director, Power, Den of Thieves, Before I Self Destruct, na The Frozen Gro.
“Nawakumbusha tu watu kwamba mwaka huu nipo vizuri, ngoma mpya, series mpya na movie mpya”, Aliandika.
50 Cent ametoa kauli hiyo kupitia ukurasa wake wa Instagram wakati akimsifia rapa Eminem juu ya taarifa ya kwamba ndiye rapa ambaye ametazamwa zaidi kwenye mtandao wa Youtube kwa mwaka 2022, akifikisha jumla ya views Bilioni 5.