
Msanii kutoka lebo ya 001 Music Happy C amefunguka kwa mara ya kwanza kuanza mazoezi ya kuinua vyuma.
Kwenye mahojiano na Lemmy Lito Sogohe, amesema imelazimika kuchukua uamuzi huo baada ya kuwa na msongo wa mawazo kutokana na kuvunjwa moyo na mpenzi wake.
Happy C ameyalaani mahusiano ya mapenzi na kusema hakuna mapenzi ya kweli.
Hata hivyo hajajulikana mrembo yupi huyo alimuumiza msanii huyo ambaye amekuwa akifananishwa na mwanamuziki wa Bongofleva Ali Kiba.