Entertainment

Msanii wa Uganda Maurice Kirya kustaafu muziki mwaka 2023

Msanii wa Uganda Maurice Kirya kustaafu muziki mwaka 2023

Msanii mkongwe kwenye muziki kutoka nchini Uganda Maurice Kirya ametangaza mpango wa kustaafu muziki.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram amewashukuru mashabiki kwa upendo ambao wamemuonesha kwa kipindi cha miaka 22 ambacho amekuwa akifanya sanaa.

Aidha amesema mwaka 2023 ndio utakuwa mwaka wa mwisho kwake kujihusisha na sanaa baada ya kukamiliasha ziara yake ya kimuziki jijini New York, London, Paris Rotterdam, Berlin, Dubai, Nairobi, Kigali na Kampala.

Hata hivyo chanzo cha karibu na msanii huyo kimesema Kirya ameechukua maamuzi hayo kwa ajili kukaa karibu na familia lakini pia kukuza biashara yake jambo ambalo litakuwa ngumu kwake kujihusisha na muziki.

Utakumbuka wasanii kadhaa Uganda akiwemo Peter Miles na Ragga Dee wanafanya muziki na biashara huku wakilea familia zao kwa wakati mmoja

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *