
Msanii wa nyimbo za injili nchini Mercy Masika ametolea uvivu wanawake wote wanaopenda kutoka kimapenzi na wanaume walio kwenye ndoa.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram Mercy amesema wanawake wa sampuli hiyo ni wavivu wa kutafuta na kuwajenga waume zao.
Amesisitiza kuwa kadhia hiyo ya uzembe na kutojali hugharimu maisha ya watu wengi kwa kuwasababishia machungu na majuto siku za mbeleni .
“People who prefer going after married people. Dont want to build. That laziness and carelessness causes so much pain in future”, Ameandika.