Mercy Masika Akiri Kupata Ugumu wa Kumpikia Mume wake

Mercy Masika Akiri Kupata Ugumu wa Kumpikia Mume wake

Mwimbaji wa nyimbo za injili kutoka Kenya, Mercy Masika, amekiri kuwa alipitia changamoto kubwa katika mwaka wake wa kwanza wa ndoa, hasa katika suala la kumpikia mume wake, akisema hali hiyo ilikuwa mshtuko kwake mwanzoni. Akizungumza kuhusu uzoefu huo, Masika amesema alijikuta akishangazwa na kuona mume wake amekaa chini akisubiri apikiwe, jambo ambalo halikuwa rahisi kulielewa kutokana na maisha aliyokuwa amezoea kabla ya ndoa na nafasi yake kama msanii mwenye umaarufu mkubwa. Mercy Masika amesema kuwa umaarufu na ratiba zake za kazi zilimfanya kuona hali hiyo kama mzigo, lakini baadaye alitambua kuwa ndoa inahitaji kujifunza, kujitoa na kubadilisha mtazamo kuhusu maisha ya ndoa na majukumu yake kama mke.

Read More
 Mercy Masika awachana wanawake wanaotembea na wanaume wa watu

Mercy Masika awachana wanawake wanaotembea na wanaume wa watu

Msanii wa nyimbo za injili nchini Mercy Masika ametolea uvivu wanawake wote wanaopenda kutoka kimapenzi na wanaume walio kwenye ndoa. Kupitia ukurasa wake wa Instagram Mercy amesema wanawake wa sampuli hiyo ni wavivu wa kutafuta na kuwajenga waume zao. Amesisitiza kuwa kadhia hiyo ya uzembe na kutojali hugharimu maisha ya watu wengi kwa kuwasababishia machungu na majuto siku za mbeleni . “People who prefer going after married people. Dont want to build. That laziness and carelessness causes so much pain in future”, Ameandika.

Read More