
Msanii kutoka nchini Kenya Vivianne yupo mbioni kuachia EP yake mpya ya nyimbo za Dini, ikiwa ni mara ya kwanza kufanya hivyo tofauti na alivyozoeleka akiimba za kidunia.
Akizungumzia ujio wa EP yake kwenye mahojiano na SPM Buzz, Vivianne amesema alikuwa na ndoto ya kutoa kazi yenye nyimbo za dini na anafurahi kuona anaenda kutimiza ndoto yake
Hata hivyo licha kutoweka wazi jina na idadi ya nyimbo zinazopatikana kwenye EP yake, amewataka mashabiki kukaa mkao kula kupokea ujio wake mpya hivi karibuni.
Utakumbuka mapema mwaka huu Vivianne alitubariki na album iitwayo Vivi iliyokuwa na jumla ya nyimbo 10 ikiwa na kolabo 3 kutoka kwa wakali kama Kidum Kibido, Trio Mio na Sosuun.