Entertainment

SHATTA WALE ATIWA MBARONI KWA KUSAMBAZA TAARIFA ZA UONGO

SHATTA WALE ATIWA MBARONI KWA KUSAMBAZA TAARIFA ZA UONGO

Jeshi la Polisi nchini Ghana limemtia mbaroni mwanamuziki Shatta Wale kwa madai ya kusambaza taarifa zisizo za ukweli kiasi cha kuzua hofu na taharuki kwa jamii. Oktoba 19 mwaka huu zilienea taarifa zikidai kuwa mwanamuziki huyo amepigwa risasi mitaa ya East Legon, nchini Ghana.

Mtu wa karibu na rapa huyo alienda mbali zaidi na kusema kwamba Shatta Wale amekimbizwa hospitali kwa matibabu. Baada ya taharuki kubwa kwa wananchi kupitia mitandao ya Kijamii, Jeshi la Polisi lilitoa tangazo la kumtafuta Shatta Wale ambaye asubuhi ya leo alifika kituoni na kujisalimisha. Polisi wamethibitisha kukamatwa kwa Shatta Wale kwa kuandika ujumbe kwenye mtandao wa Facebook.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *