Entertainment

Willy Paul adai umaarufu umemnyima uhuru mtaani

Willy Paul adai umaarufu umemnyima uhuru mtaani

Hitmaker wa “Tamu Wallahi”, Msanii Willy Paul amedai kwamba stress ya umaarufu imemnyima uhuru wa kutembea mitaani na kufanya shughuli zake kwa amani.

Hii ni baada ya watu wasiojulikana kumvamia na kumdhalilisha akiwa Casavara Lounge Jijini Nairobi ambako alienda kuwachukua marafiki zake waliokuwa wamekwama katika chimbo hilo la burudani.

Kupitia instastory yake ameandika ujumbe wa masikitiko akieleza namna watu wamekuwa wakitumia jina lake kujitakia makuu huku akiwataka mashabiki kutomuona wa kitofauti kwani yeye ni binadamu wa kawaida kama watu wengine.

Aidha ameenda mbali na kujinasibu kuwa anashukuru Mungu kumpa moyo wa kutolipiza kisasi kipindi ambacho watu wanamvunjia heshima kwa kumshushia matusi na taarifa za uongo mtandaoni.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *