Entertainment

Magix Enga apata ukosoajii mkubwa mtandaoni kwa kujihusisha na kiki

Magix Enga apata ukosoajii mkubwa mtandaoni kwa kujihusisha na kiki

Prodyuza asiyeishiwa na matuko kila leo Magix Enga amejipata njia panda mtandaoni mara baada ya walimwengu kumshambulia kwa kuendekeza kiki kwenye sanaa yake.

Purukushani ya wakenya na Magix ilianza pale ambapo prodyuza huyo aliposti picha akiwa kaunti ya Kilifi kwenye shughuli za kuinua vipaji siku chache baada ya video yake akiwa mlevi chakari kusambaa mtandaoni ambapo watu wengi walihuzunishwa na kisa hicho, wakitoa rai kwa wahisani kujitokeza na kumsaidia prodyuza kutokana na uraibu wa pombe ulioathiri maisha.

Watumiaji wengi wa mitandao ya kijamii wameonekana kukerwa na sarakasi za prodyuza huyo kwa kumshushia kila aina ya matusi huku wakimtaka aache kutengeneza kiki zisizo kuwa na mashiko kwa lengo la kutangaza kazi zake.

Aidha baadhi wamehoji kuwa kitendo cha Enga kuishi maisha ya kuigiza mitandaoni itagharimu siku za mbeleni kwani watu wataanza kumchukulia poa ikitokea amepatwa na tatizo.

Hii sio mara ya kwanza kwa Magix Enga kujihusisha na kiki zenye utata, miezi kadhaa iliyopita alikiri kuwa mwanachama wa dhehebu la IIlluminati, madai ambayo baadaye alikuja akajitenga nayo kwa kusema alikuwa anatafuta mazingira ya kuzungumziwa kwenye tasnia ya muziki nchini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *