
Mashabiki wa Rapa Tory Lanez, wameanzisha kampeni ya kushinikiza ombi la kukataa rufaa baada ya kutoridhishwa na maamuzi ya mahakama kwa rapa huyo katika kesi yake ya kumshambulia risasi Megan Thee Stallion Julai mwaka 2020.
Mpaka sasa ombi hilo limefikisha zaidi ya saini 30,000 .
Hatua hii imekuja siku chache kufuatia ya timu ya Tory Lanez kuonekana kutoridhishwa na maamuzi ya mahakama, ambapo wakili wake George Mgdesyan alidai anapanga kukata rufaa dhidi ya hukumu hiyo kwani hakuna ushahidi uliojitosheleza.
Tory Lanez atabaki rumande akingoja hukumu yake kusomwa Januari 27, mwaka 2023 baada ya kukutwa na hatia kwenye mashtaka matatu ikiwemo kumshambulia Megan kwa kutumia silaha lakini pia kubeba silaha iliyopakiwa risasi na ambayo pia haijasajiliwa.