Entertainment

Rapa King Kaka ahirisha kuachia ya Album yake mpya

Rapa King Kaka ahirisha kuachia ya Album yake mpya

Rapa kutoka nchini Kenya King Kaka ametangaza kutoachia Album yake mpya kama alivyoahidi hapo awali kuwa itatoka Desemba 25.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Bosi huyo wa Kaka Empire, amesema kutokana na ukubwa wa Album hiyo Uongozi wake umependelea itoke mwaka 2023 kwa sababu kuna wimbo wa msanii kutoka Jamaica ambao unapaswa kujumuisha kwenye album yake mpya.

Rapa huyo amewaomba radhi mashabiki zake kwa kuchelewesha mchakato wa kuachia Album yake aliyoipa jina la β€œ2nd Life” huku akiwashukuru kwa upendo ambao wamekuwa wakimuonyesha kwa miaka mingi.

Album hiyo ambayo ni ya tano katika safari yake ya muziki ina jumla ya mikwaju 17 ya moto kutoka kwa wakali kama Wanavokali, Femi One, Iyaniii, Kanambo Dede,Solomon Mkubwa, Goodluck Gozbert na wengine wengi.

2nd Life ni Album ambayo King Kaka ameamua kuachia kwa ajili ya kumrudishia Mwenyezi Mungu fadhila kwa kumpa nafasi nyingine ya kuishi duniani ikizingatiwa kuwa mwaka 2021 nusra ampoteze maisha yake baada ya kuugua ugonjwa usiojulikana uliofanya kupoteza uzani wa kilo 33.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *