
Mwakilisha wa tamasha la SoFire Fiesta amejibu malalamishi ya msanii Stevo Simple Boy ya kutolipwa kwenye show huko Mombasa
Kwenye mkao na wanahabari amethibitisha kuwa Stevo alipewa nafasi ya kutoa buradani kwenye shoo hiyo lakini hakufanikiwa kufanya hivyo kutokana na uongozi wake kuwa kizingiti.
Aidha amesema kuwa hakuwa anasimamia wasanii wa Kenya kwenye masuala ya malipo kwa kuwa alikuwa na majukumu mengine ya kuhakikisha wasanii wa kigeni wanalipwa kwa wakati unaofaa.
Hata hivyo amesema hawakuwa na mkataba wa kufanya kazi na stevo licha ya kumpa nafasi kutumbuiza kwenye shoo hiyo huku akisisitiza kuwa wangemlipa pesa zake iwapo angepanda jukwaani kuwapa mashabiki waliohudhuria burudani.
Kauli yake hiyo imezua maswali mengi miongoni mwa wa Kenya kama ilivyotakiwa huku wakionyoshea kidole cha lawama mapromota kwa kuwapa kipau mbele wasanii wa kigeni huku wakiwachukulia poa wasanii wa ndani.