Entertainment

Anjella awataka mashabiki wawe na subira

Anjella awataka mashabiki wawe na subira

Mwimbaji Anjella  baada ya kuaga Konde Music Worldwide amewataka mashabiki wake wawe na subira.

Nyota huyo wa kizazi kipya amebainisha hilo akizungumza kwenye mahojiano na CloudsE ya Clouds Fm mchana huu.

“Kila kitu nitakuja kukiweka wazi, mashabiki wangu wawe na subira,” -ameeleza Anjella akiiambia Clouds E.

Anjella ameamua kueleza hilo kufuatia mashabiki wake kutamani kujua hatma yake ama nini kifuatacho kutoka kwake baada ya kuachana na Konde Gang.

Itakumbukwa, Anjella alitambulishwa kwenye lebo ya Konde Music Worldwide Machi 11, 2021, hadi anaaga leo hii, Januari 02, 2023 anakuwa amedumu kwenye lebo hiyo kwa muda wa mwaka mmoja na miezi tisa

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *