Entertainment

Justina Syokau angua kilio kutokana na chuki anayopata kutoka kwa mashabiki

Justina Syokau angua kilio kutokana na chuki anayopata kutoka kwa mashabiki

Mwanamuziki wa Injili Justina Syokau ameumizwa na chuki ambayo amekuwa akiipata hasa baada ya kuachia wimbo wake mpya ‘Twendi Twendi Thilii’.

Akizungumza katika mahojiano, Justina Syokau amesema alirekodi wimbo huo chini ya shinikizo ya Roho Mtakatifu lakini Wakenya wameitafsiri vibaya dhana ya wimbo huo.

Mwanamuziki huyo ambaye alikuwa akitokwa na machozi akielezea maana ya ujumbe, 2023 ni mwaka wa kupanuliwa, amesema watu ambao hawana ushawishi wa roho mtakatifu watauelewa wimbo huo kwa maana ya kidunia ambayo haikuwa dhamira ya wimbo wake.

“Nyimbo zangu ni unabii na ukiziamini mambo yako yatatimia. Magavana wamekuwa wakinipigia simu baada ya wimbo wangu wa 2022. Waliamini maneno hayo na wakachaguliwa.”

Justina Syokau amesema amechoka kuimba kutokana na watu kutothamini nyimbo zake na 2023 ni mwaka wa mwisho kutoa wimbo kwani ameamua kufungua kanisa lake na kuwa nabii.

“Badala ya Wakenya kuthamini kwamba wana nabii, wamekuwa wakinisema vibaya. Sijui ama nianze kanisa. Mbona hamtaki nisonge mbele, nikiimba Hamnitakii, mnataka niwafanyie nini, mnahangaika mnaomba kila siku ili nipate maudhui ya kuweka hapo, mnaomba mnipe kazi mnaendelea kunitusi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *