
Rapa kutoka nchini Tanzania Country Wizzy ameweka wazi kuja na sehemu ya pili ya album yake ya Yule Boy ambapo sehemu ya kwanza ya album hiyo ilitoka mwaka 2019 ikiwa na jumla ya ngoma 30.
Kupitia ukurasa wake wa Twitter, ametangaza kuwa ni muda wa studio sasa kwa ajili ya kuandaa sehemu ya pili ya album ya Yule Boy.
“Studio time for Yule Boy Album Part 2…, see yall when the music is ready”, Aliandika.
Itakumbukwa, sehemu ya kwanza ya album ya Yule Boy iliwakutanisha wakali wengine kama Moni Centrozone, Harmonize, Mwana FA, Khaligraph Jones, G Nako, na Mimi Mars.