
Msanii Nadia Mukami amejitokeza na kukanusha madai kwamba Saloon iliyozinduliwa hivi karibuni imefadhiliwa na mdhamini, na kwamba yeye ni wakala tu wa kutangaza Saloon hiyo.
Akizungumza na Nairobi news, Nadia amefichua kuwa saloon iliyofunguliwa mwezi Disemba 2022 ni jasho lake na timu yake inaweza kuthibitisha hilo.
“Siku zote watu watanikosoa kwa njia mbaya, wengine watadai nimedhaminiwa lakini ni timu yangu tu na wale walio karibu nami wanaelewa mapambano niliyopitia kuzindua saloon hii,” Nadia alisema akijibu madai hayo.
Msanii huyo amesimulia mapambano aliyopitia akijaribu kutafuta fedha za kufungua biashara hiyo na kuwatolea uvivu wanaodai kuwa yeye sio mmiliki halisi wa saloon hiyo kwa kusema kuwa mradi huo ulimgharimu zaidi ya shilingi milioni 1.2 za Kenya na zote zilitokana na fedha za akiba.
“Kwa wale wanaofuata kile ninachofanya, wananiona nikifanya shows, juzi nilifanya moja na Safaricom na nililipwa vizuri.
Nimekuwa nikifanya kazi na EABL kwa muda mrefu zaidi. Namaanisha kwa nini mtu afikirie siwezi kumudu gharama ya kuanzisha biashara kama hiyo?” Mwanamuziki huyo alisema akionekana kukerwa na madai ya walimwengu.
Hata hivyo amewaambia mashabiki zake kwamba licha ya kutotoa vibao vingi mwaka 2022, ana mengi ya kufanya mwaka huu ikiwemo kuachia Album mpya.