
Mkongwe wa muziki wa Bongo Fleva, Seleman Msindi maarufu ‘Afande Sele’ amezijia juu Klabu za Simba na Yanga kwa kuzitaja kama makaburi ya Soka la Bongo.
Afande Sele ametumia ukurasa wake wa Instagram akieleza kwenye andiko lake ambapo akizilaumu Simba na Yanga kwa kusema zimekua zikiua Soka la Tanzania na akaenda mbali zadi kwa kutoa shutuma za kupanga matokeo kwa kununua wachezaji wa timu pinzani na waamuzi, ili kushinda michezo ya Ligi Kuu Tanzania Bara, eti kwa kisingizio cha kuwa Mabingwa.
Mkongwe huyo pia amegusia suala la Simba kumleta Kocha Mkuu mpya kutoka nchini Brazil, Roberto Oliveira Gonçalves do Carmo ‘Robertinho’, ili hali tayari wamekua na Kocha Mzawa Juma Mgunda, ambaye ameonesha kuwa na mustakabali mzuri wa kuipa matokeo timu katika Michuano ya Kimataifa na ile ya ndani ya Tanzania Bara.
Afande Sele yeye anaona Simba haikuwa na sababu ya kuchukua Kocha wa nje wakati huu, anasema hatoshangaa kuona timu ikivurugika na kupoteza mwelekeo zaidi badala ya kuimarika