Entertainment

Mwanamitindo akutwa amefariki Kenya

Mwanamitindo akutwa amefariki Kenya

Polisi katika kaunti ya Uasin Gishu wanachunguza chanzo cha mauaji baada ya mwili wa mwanamitindo maarufu Edwin Chiloba kukutwa umetupwa ukiwa ndani ya sanduku la chuma.

Kulingana na chanzo kimoja cha habari ,mwendesha Bodaboda aliona gari ambalo halikuwa na namba likitupa sanduku la chuma kando ya barabara ya Kipenyo – Kaptinga.

Kisa hicho kiliripotiwa kwa polisi wa Uasin Gishu ambao walifika eneo la tukio na walipofungua sanduku hilo, walikuta mwili wa mwanamume aliyekuwa amevalia nguo za kike uliokuwa ukianza ukioza. Baadaye ilibainika kuwa marehemu alikuwa mbunifu wa mitindo wa Eldoret Edwin Chiloba.

Mwili huo ulipelekwa katika hospitali ya rufaa ya Moi ukisubiri uchunguzi wa maiti kubaini chanzo cha kifo hicho.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *