Entertainment

Willy Paul awajia juu wanablogu wa Kenya kwa kutangaza wasanii wa kigeni

Willy Paul awajia juu wanablogu wa Kenya kwa kutangaza wasanii wa kigeni

Msanii asiyeishwa na matukio kila leo, Willy Paul ameamua kuwachana mablogger wa Kenya kwa kile anachodai kuwa wamekosa uzalendo kwenye mchakato mzima wa kuwaunga mkono wasanii wa ndani (local artistes).

Kupitia instastory yake ametoa ya moyoni kwa kusema kuwa njaa ya pesa imewaponza wanablogu wa humu nchini kiasi cha kuanza kutangaza sana muziki wa kigeni kwenye mitandao yao ya kijamii ilhali Kenya kuna wasanii wengi wenye vipaji.

Bosi huyo wa “Saldido” amesema tatizo hilo lisipopata mwarubaini huenda tasnia ya muziki nchini ikapoteza mwelekeo kwani ma-blogger wa Kenya wamerubuniwa na mapromota wa nje ambao wamekuwa wakiwahonga mkwanja mrefu ili wawape wasanii wao kipau mbele kwenye majukwaa tofauti mtandaoni.

Hata hivyo ametoa changamoto kwa wasanii kuamka na kupambania kazi zao ziwafikie watu wengi duniani kutokana na usaliti ambao wameoneshwa na wakenya wenzao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *