
Hukumu ya Tory Lanez imesogezwa mbele kutoka Januari 27 na sasa itatoka Februari 28 mwaka huu. Wiki iliyopita Tory Lanez alimfukuza kazi mwanasheria wake na kumuajiri mpya (David Kenner) ambaye ana uzoefu na mashtaka ya jinai.
wakili huyo “David Kenner” ambaye ana uzoefu katika kesi za jinai aliwahi pia kumsaidia rapa Snoop Dogg kwenye kesi yake ya mauaji mwaka 1993.
Utakumbuka mwaka jana Tory alikutwa na hatia ya makosa yote matatu ambapo kifungo chake ni zaidi ya miaka 22 jela. Tory Lanez hadi sasa amebaki rumande akisubiri hukumu yake ambayo itasomwa Februari 28, mwaka 2023.