
Mkali wa michano kutoka Marekani Kendrick Lamar anaweza kudondosha album yake mpya kesho Ijumaa.
Hii imekuja kufuatia kuvuja kwa ngoma iitwayo “Therapy Session 9” lakini pia mabadiliko ya picha ya Kendrick Lamar kwenye mtandao wa Spotify.
Ni miaka minne tangu Kendrick Lamar asikike kwa upana kwenye masikio ya mashabiki zake kupitia album yake ya mwisho iitwayo DAMN iliyotoka mwaka 2017. Hivi karibuni alikuja na tamko la ujio wa album mpya na ya mwisho kwenye label yake ya Top Dawg Entertainment ambayo aliitumikia kwa miaka 17.