
Mwimbaji nyota nchini, Jovial amethibitisha rasmi ujio wa EP yake mpya na ya kwanza katika safari yake ya muziki.
Kupitia Instastory yake ameweka wazi mpango wake huo huku akisema kuwa amekamilisha mchakato wa kuiandaa EP hiyo.
Lakini pia ameeleza kwamba, wimbo wa kwanza kutoka kwenye EP yake itaingia sokoni wiki mbili zijazo.
Hata hivyo mrembo huyo bado hajaweka wazi jina na idadi ya nyimbo zitakazopatikana kwenye EP yake hiyo.