Entertainment

John Legend na mkewe Chrissy Teigen wamebarikiwa kupata mtoto

John Legend na mkewe Chrissy Teigen wamebarikiwa kupata mtoto

Mwanamuziki kutoka Marekani ambaye pia ni mshindi wa Tuzo ya Grammy John Legend na mkewe Chrissy Teigen wamebarikiwa kupata mtoto mwingine.

Kwa mujibu wa Jarida la People, Teigen alijifungua JanuarI 13, mwaka 2023.

Legend pia alitangaza taarifa hiyo njema kupitia onesho lake binafsi ambapo aliwaambia wahudhuriaji kwamba “The little baby this morning. What a blessed day.”

Familia yao imeongezeka sasa, kwani wana watoto wawili wakubwa, Luna na Miles.

Ikumbukwe mwezi Oktoba mwaka 2020 wawili hao waliitia dunia nzima kwenye majonzi baada ya tukio la kumpoteza mtoto wao (Jack) kufuatia Teigen kupata tatizo la kuharibika kwa ujauzito akiwa kwenye kitanda cha kujifungulia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *