
Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Platform, ameeleza kuwa hupata wivu simu ya mpenzi wake ikiita na kutamani kufahamu ni nani amepiga.
Kupitia ukurasa wake wa kijamii wa instagram ameandika ‘’Kwa upande wangu #Wivu wangu kwa mpenzi wangu ni simu yaani simu ikiita tuuu lazima niangalie nani kapiga. “Je wewee una #Wivu kama wangu???? “Save Date 20.1.2023:”
Ujumbe wake huo umetafsiriwa na wajuzi wa mambo huenda msanii huyo ana mpango wa kuachia wimbo mpya uitwao “Wivu” Januari 20 mwaka huu.
Hata hivyo ngoma ya mwisho kwa Platform kutoa kwa mwaka 2022 ilikuwa ni “Nileweshe” ambayo ina watazamaji elfu 10,395.