
Rapa kutoka nchini Tanzania Stamina ametangaza kuuanza mwaka 2023 kwa ukubwa zaidi pamoja na maandalizi ya album.
Stamina amebainisha hilo kupitia ukurasa wake wa Instagram, akieleza habari hiyo njema kwa mashabiki wake ikiwa mwaka 2022 aliumaliza kwa kishindo.
“Habari njema ni kwamba, nipo tayari kuuanza mwaka huu mpya kwa project nzito nzito na album kabisa. Kaa tayari nipo njiani 💪.” – Aliandika.
Stamina katika safari yake ya muziki tayari ana album moja iitwayo PARADISO aliitoa mwaka 2021, na hii mpya inaenda kuwa album yake ya pili.