Stamina atangaza kufanya makubwa mwaka 2023

Stamina atangaza kufanya makubwa mwaka 2023

Rapa kutoka nchini Tanzania Stamina ametangaza kuuanza mwaka 2023 kwa ukubwa zaidi pamoja na maandalizi ya album. Stamina amebainisha hilo kupitia ukurasa wake wa Instagram, akieleza habari hiyo njema kwa mashabiki wake ikiwa mwaka 2022 aliumaliza kwa kishindo. “Habari njema ni kwamba, nipo tayari kuuanza mwaka huu mpya kwa project nzito nzito na album kabisa. Kaa tayari nipo njiani 💪.” –  Aliandika. Stamina katika safari yake ya muziki tayari ana album moja iitwayo PARADISO aliitoa mwaka 2021, na hii mpya inaenda kuwa album yake ya pili.

Read More
 Stamina ashinda Tuzo ya Msanii bora wa Hiphop Afrika Mashariki

Stamina ashinda Tuzo ya Msanii bora wa Hiphop Afrika Mashariki

Rapa kutoka Tanzania Stamina ameshinda tuzo ya Msanii Bora wa Rap/Hip Hop Afrika Mashariki kwenye Tuzo za Platform show 257 za nchini Burundi. Kwenye kipengele hicho alikuwepo pia Rapa wa Kenya Khaligraph Jones, Rosa Ree wa Tanzania, B-Face wa Burundi na Ish Kevin wa Rwanda. Stamina hata hivyo hakuweza kuhudhuria kwenye hafla ya utowaji wa tuzo hizo kwa kuwa ratiba yake iliingiliana na show yake ya Fiesta ya Jijini Mwanza, Tanzania.

Read More