
Msanii kutoka nchini Nigeria, CKay anaendelea kuweka rekodi kupitia wimbo wake (Love Nwantiti) ambao ulitoka mwaka 2020.
Kwa mujibu wa Recording Industry Association of America (RIAA), wimbo huo umegonga Platinum 4 yaani umeuza zaidi ya nakala milioni 4.
Utakumbuka Januari 11 mwaka huu Ckay aliandika rekodi nyingine kubwa ambapo wimbo huo ulitajwa namba moja kwenye orodha ya nyimbo za kiafrika zilizouza zaidi nchini Marekani mwaka 2022, ukiingiza zaidi ya KSh. millioni 198.