Entertainment

Lily Wayne akataa utajiri kutumika kama ushahidi mahakamani

Lily Wayne akataa utajiri kutumika kama ushahidi mahakamani

Rapa kutoka nchini Marekani Lil Wayne amedai kwamba hali yake ya kifedha inapaswa kuachwa mbali na kesi ya madai ya ushambulizi dhidi ya msaidizi wake wa zamani, Andrew Williams ili isije kuathiri mchakato wa mahakama.

Rapa huyo Anataka taarifa kuhusu utajiri wake kuepukwa isipokuwa tu kama atapatikana na hatia, kwa kudai kuwa kuhusisha mambo ya kifedha kabla ya hukumu kunaweza kumshawishi jaji kwa namna isiyo ya haki.

Pia, Lil Wayne amepinga ombi la Williams la kukutana uso kwa uso, akisema kwamba anapaswa kupewa nafasi ya kutoa taarifa kwa mbali kama ilivyokuwa kwa Williams. Kesi hiyo inaendelea, huku Lil Wayne akitaka kuiondoa kabisa na kuomba mahakama kumlipa.

Kesi hiyo inahusisha tukio la mwaka 2022, ambapo Williams anadai kwamba alishambuliwa na Lil Wayne kwa kumpiga ngumi wakati walipokuwa kwenye ndege binafsi baada ya mzozo kati ya Lil Wayne na rubani.

Williams anasema kwamba alijaribu kutuliza hali hiyo, lakini alishambuliwa kwa ngumi zilizohusisha pete na mapambo ya dhahabu ya mikononi mwa Lil Wayne, na alidai kwamba alijeruhiwa vibaya.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *