Entertainment

Jennifer Lopez Akumbwa na Kesi ya Haki Miliki kwa Kuposti Picha za Paparazzi Bila Ruhusa

Jennifer Lopez Akumbwa na Kesi ya Haki Miliki kwa Kuposti Picha za Paparazzi Bila Ruhusa

Mwanamuziki na muigizaji nyota wa Marekani, Jennifer Lopez, anakabiliwa na madai ya ukiukaji wa haki miliki baada ya kuripotiwa kuposti picha mbili za paparazzi bila kulipia leseni ya matumizi.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Billboard, picha hizo zilipigwa wakati Lopez alipokuwa nje ya hafla ya tuzo za Golden Globes mwezi Januari,na baadaye kupostiwa kwenye akaunti yake ya mitandao ya kijamii. Hata hivyo, shirika linalomiliki picha hizo linadai kuwa Lopez hakununua haki za kuzitumia, jambo ambalo linakiuka sheria za hakimiliki.

Hadi sasa, Jennifer Lopez au wawakilishi wake hawajatoa taarifa rasmi kuhusu tuhuma hizo.

Madai hayo yanaongeza msururu wa kesi zinazowakumba mastaa mbalimbali wa Hollywood kwa kutumia picha za paparazzi bila ruhusa, licha ya wao kuwa wahusika wakuu kwenye picha hizo.

Kesi hii inaibua tena mjadala mpana kuhusu mipaka ya haki miliki katika enzi ya mitandao ya kijamii, ambapo mastaa wengi huchukulia kuwa picha zao binafsi zinaweza kutumika bila masharti jambo ambalo kisheria haliko wazi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *