Sports news

Real Madrid Waagana na Luka Modric Baada ya Miaka 13 ya Mafanikio

Real Madrid Waagana na Luka Modric Baada ya Miaka 13 ya Mafanikio

Klabu ya Real Madrid jana imeaga rasmi kiungo wao nyota Luka Modric, baada ya kulitumikia kikosi hicho kwa miaka 13. Modric alijiunga na Madrid mwaka 2012 akitokea Tottenham Hotspur ya England, na tangu wakati huo amekuwa sehemu muhimu ya mafanikio ya Los Blancos.

Miongoni mwa mafanikio makubwa ya Modric akiwa Madrid ni pamoja na kutwaa Ballon d’Or mwaka 2018, na kushinda mataji sita ya Ligi ya Mabingwa Ulaya (UEFA Champions League). Mchango wake katika safu ya kiungo umeisaidia Madrid kutawala soka la Ulaya kwa kipindi kirefu.

Modric pia anasifika kwa uongozi, nidhamu, na ustadi wa hali ya juu ndani ya uwanja, akiwa mfano bora kwa wachezaji chipukizi. Kuondoka kwake kumeacha pengo kubwa lakini pia kumbukumbu ya mafanikio ya kipekee katika historia ya klabu hiyo.

Katika mechi ya mwisho ya msimu, Real Madrid waliibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya Real Sociedad, ambapo mashabiki walimshangilia Modric kwa heshima kubwa, wakimpa kwaheri ya kipekee kwa mchango wake mkubwa kwa miaka yote aliyovaa jezi nyeupe ya Madrid.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *