
Mckekeshaji maarufu nchini Kenya, 2Mbili, amewaacha mashabiki wake na huzuni na mshangao baada ya kufichua kupitia ukurasa wake wa Instagram kuwa alivamiwa na watu wasiojulikana alipokuwa kwenye foleni ya magari, karibu kabisa na eneo lililotokea ajali mbaya iliyogharimu maisha ya abiria kadhaa.
Katika ujumbe huo uliojaa hisia, msanii huyo alieleza kuwa alipigwa jicho lake la kulia kwa nguvu kiasi kwamba anaumia sana, hasa anapokutana na mwangaza. Ameeleza kuwa anaendelea kuvumilia maumivu huku akisisitiza kuwa ana nia ya kuendelea na maisha na kazi yake bila kukata tamaa.
βKuna majamaa walinivamia kwa traffic. Just metres from the tragic accident that had killed a few of the passengers! One guy hit my right eye so hard. The pain is something else especially kwa light. Mniombee. Najikaza sana coz mimi lazima nitokelezee!! Whats behind those shades is crazy, natoa shades every minute kupanguza machozi!! Hii
Β ndo emoji yangu sahiΒ
β Aliandika na maumivu na hisia kali Instagram.
Mashabiki na wafuasi wake mitandaoni wamejitokeza kwa wingi kumpa pole na kumtakia afueni ya haraka, huku wengine wakielezea wasiwasi wao juu ya usalama wa wasanii mitaani.
Tukio hili linazua maswali kuhusu usalama wa raia, hasa wakati wa foleni ndefu za magari ambapo visa vya uhalifu hufanyika bila kutarajiwa. Mashabiki wengi wanatumai kuwa 2mbili atapata nafuu haraka na kurejea tena katika hali yake ya kawaida ya burudani.