
Msanii maarufu wa muziki nchini Uganda, Bebe Cool, amefunguka kuhusu maswali yanayoendelea kuibuka kuhusu uwekezaji mkubwa alioufanya katika utengenezaji wa album yake mpya yenye nyimbo 16. Msanii huyo amefichua kuwa amewekeza zaidi ya dola 700,000 za Kimarekani kwenye mradi huo.
Akizungumza na waandishi wa habari, Bebe Cool, ambaye jina lake halisi ni Moses Ssali, amesisitiza kuwa kiasi hicho cha fedha kimetumika ipasavyo kuhakikisha ubora wa hali ya juu wa album hiyo.
Msanii huyo hakusita kuwajibu wale wanaotia shaka kiasi hicho cha fedha, akieleza kuwa gharama hizo zinajumuisha mambo mengi kuanzia kurekodi nyimbo katika studio za kisasa, malipo kwa watayarishaji wa muziki (producers) maarufu, uhandisi wa sauti (audio engineering), video za muziki zenye ubora wa hali ya juu, pamoja na gharama za masoko na matangazo.
Album hiyo ya nyimbo 16 inatarajiwa kuzinduliwa hivi karibuni, na tayari imezua hamasa kubwa miongoni mwa mashabiki wake na wadau wa muziki. Bebe Cool ana matumaini kuwa uwekezaji huu utalipa na kumpa nafasi nzuri zaidi kwenye tasnia ya muziki ya kimataifa..