
Msanii mkongwe nchini Nyota Ndogo amekanusha madai kuwa anatumia hirizi kuwarubuni wanaume wa kizungu na kufanikisha biashara zake nyingi.
Akijibu shabiki aliyemshutumu kuwa amekuwa akiwatembelea ‘waganga’ ili awavutie wanaume maishani mwake kupitia ukurasa wake wa Instagram, Nyota Ndogo amesema kuwa kwa upande wake hana imani na mambo ya kishirikina kwani anamuamini mungu kama mganga wake mkuu katika maisha yake.
Hitmaker huyo wa “Watu na Viatu” amekiri kuwa DM yake kwenye mtandao wa Instagram imejaa jumbe za watu wanaomwomba awasaidie waweze kumfikia mganga ambaye amekuwa akimsaidia kufanikisha baadhi ya mambo yake.